Monday, June 27, 2016


Mchezaji wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Barcelona Lionel Messi amejiuzulu soka la kimataifa.
          Mchezaji huyo bora zaidi duniani alitangaza hatua hiyo baada ya kukosa penalti iliyoiwezesha Chile kuilaza Argentina katika fainali ya mchuano wa Copa America.
"Kwangu mimi ,soka ya kimataifa ama hata kuichezea Argentina sitaweza tena.
''Nimefanya kila niwezalo.''
''Kwa kweli inaniumiza kuwa sijawahi kutwaa kombe lolote la kimataifa'' alisema mshambulizi huyo mwenye umri wa mia 29.
Mshambulizi huyo ameisaidia mabingwa wa ligi kuu ya Uhispania Barcelona, kutwaa mataji 8 na mataji manne ya ubingwa wa bara ulaya.
Hata hivyo kimataifa Messi amewahi kushinda taji moja tu lile la nishani ya dhahabu ya Olimipiki ya mwaka wa 2008 Olympic.

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive

Powered by Blogger.

Featured Post Via Labels

Featured Slides Via Labels

Featured Posts Via Labels

More on

Recent Posts

Popular Posts