Michuano ya Copa America imefikia tamati leo hii kwa mabingwa watetezi Chile kuendeleza ubabe wake dhidi ya Vigogo wa soka duniani Argentina.\
Monday, June 27, 2016
7:16 AM
Frank Lungwa
No comments
6:57 AM
Frank Lungwa
No comments
Mchezaji wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Barcelona Lionel Messi amejiuzulu soka la kimataifa.
Mchezaji huyo bora zaidi duniani alitangaza hatua hiyo baada ya kukosa penalti iliyoiwezesha Chile kuilaza Argentina katika fainali ya mchuano wa Copa America.
"Kwangu mimi ,soka ya kimataifa ama hata kuichezea Argentina sitaweza tena.
''Kwa kweli inaniumiza kuwa sijawahi kutwaa kombe lolote la kimataifa'' alisema mshambulizi huyo mwenye umri wa mia 29.
Mshambulizi huyo ameisaidia mabingwa wa ligi kuu ya Uhispania Barcelona, kutwaa mataji 8 na mataji manne ya ubingwa wa bara ulaya.
Hata hivyo kimataifa Messi amewahi kushinda taji moja tu lile la nishani ya dhahabu ya Olimipiki ya mwaka wa 2008 Olympic.
6:51 AM
Frank Lungwa
No comments

Afrika Kusini ilichukua nafasi ya kwanza katika mashindano ya riadha barani afrika, yaliyokamilika hiyo jana mjini Durban kwa medali 33 zikiwemo za dhahabu 16.
Mashindano hayo huwaleta pamoja wanariadha bora kutoka Afrika lakini nyota wengei wa riadha hawakushiriki.
Rais wa mashindano hayo tayari amesema kuwa wanariadha ambao watasusia mashindani ya mwaka 2018 mjini Lagos Nigeria, huenda wakazuiwa kuwakilisha nchi zao katika mashindano ya kimataifa.
Subscribe to:
Posts (Atom)

