Monday, July 4, 2016

         mshambuliaji wa  Marseille ya ufaransa Michy Batshuayi (23)ametia saini mkataba wa miaka mitano kuichezea Chelsea inayoongozwa na kocha Antonio conte.michy anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na klabu na meneja huyo mpya alishika nafasi ya Jose mourinho ambaye alitimuliwa kutokana na klabu hiyo kuwa na mwenendo mbaya katika ligi ya EPL.Mchezaji huyo aliyeigharimu Chelsea Euro milioni 40 ana asili ya kutoka nchi ya Congo lakini kwa sasa amechagua kuichezea timu ya taifa ya UBELGIJI.

Monday, June 27, 2016

    Michuano ya Copa America imefikia tamati leo hii kwa mabingwa watetezi Chile kuendeleza ubabe wake dhidi ya Vigogo wa soka duniani Argentina.\

Dakika 120 za mchezo huo zilishuhudia timu hizo zikienda suluhu ya bila kufungana. Mchezo huo ulitawaliwa na ubabe wa hapa na pale huku ikushuhudiwa timu zote mbili zikimaliza kipindi cha kwanza zikiwa na wachezaji 10 baada ya Marcelo Diaz wa Chile kulambwa kadi mbili za njano na kuwa nyekundu dakika ya 28 kabla ya Marcos Rojo wa Argentina kutolewa nje dakika ya 43 kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja. Katika upigaji wa penalti,Arturo Vidal wa Chile alianza kwa kukosa kabla ya Lionel Messi na Lucas Biglia kukosa kwa upande wa Argentina. Hii inakuwa fainali ya pili ndani ya miaka miwili kwa timu hizi mbili kukutana katika hatua ya fainali amapo mara zote mbili Chile wamechukuwa kikombe hicho kwa mikwaju ya penalti. Fainali hizi zilichezwa mwaka jana nchini Chile na kurudiwa mwaka huu ikiwa ni maadhimisho ya miaka 100 tokea kuanza kwa michuano hii mwaka 1916.




Mchezaji wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Barcelona Lionel Messi amejiuzulu soka la kimataifa.
          Mchezaji huyo bora zaidi duniani alitangaza hatua hiyo baada ya kukosa penalti iliyoiwezesha Chile kuilaza Argentina katika fainali ya mchuano wa Copa America.
"Kwangu mimi ,soka ya kimataifa ama hata kuichezea Argentina sitaweza tena.
''Nimefanya kila niwezalo.''
''Kwa kweli inaniumiza kuwa sijawahi kutwaa kombe lolote la kimataifa'' alisema mshambulizi huyo mwenye umri wa mia 29.
Mshambulizi huyo ameisaidia mabingwa wa ligi kuu ya Uhispania Barcelona, kutwaa mataji 8 na mataji manne ya ubingwa wa bara ulaya.
Hata hivyo kimataifa Messi amewahi kushinda taji moja tu lile la nishani ya dhahabu ya Olimipiki ya mwaka wa 2008 Olympic.

     Afrika Kusini ilichukua nafasi ya kwanza katika mashindano ya riadha barani afrika, yaliyokamilika hiyo jana mjini Durban kwa medali 33 zikiwemo za dhahabu 16.
Kenya ilipata medali 24 zikiwmo 8 za dhahabu.
Mashindano hayo huwaleta pamoja wanariadha bora kutoka Afrika lakini nyota wengei wa riadha hawakushiriki.
Kenya ilituma wanariadha wa tajriba ya chini bila kutuma nyota yeyote hatua ambayo pia ilichukuliwa na Ethiopia
Rais wa mashindano hayo tayari amesema kuwa wanariadha ambao watasusia mashindani ya mwaka 2018 mjini Lagos Nigeria, huenda wakazuiwa kuwakilisha nchi zao katika mashindano ya kimataifa.

Blog Archive

Powered by Blogger.

Featured Post Via Labels

Featured Slides Via Labels

Featured Posts Via Labels

More on

Recent Posts

Popular Posts